Monday, March 23, 2015



Na Bertha Lumala, Tanga
Wakati Simba SC ikisahihisha makosa ya Jumatano kwa kuichapa Ruvu Shooting Stars Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Azam FC nao wametakata kwa kuilamba bao 1-0 Coastal Union FC Uwanja wa Mkwakwani jijini hapa jana jioni.

Bao pekee la mechi hiyo iliyokuwa ngumu na iliyosheheni ushindani, limefungwa na mshambuliaji mkongwe na Nahodha wa Azam FC, John Bocco 'Adebayor' dakika ya 31 akiitendea haki pasi maridhawa iliyopenyezwa ndani ya boksi na kiungo fundi Mudathiri Abbas Yahya.

Kwa matokeo hayo, Azam FC inayonolewa na Mganda George Nsimbe baada ya kutimuliwa kwa Mcameroon Joseph Omog, imeendelea kubaki nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu ya Bara ikifikisha pointi 36, moja nyuma ya vinara Yanga SC baada ya timu zote kucheza mechi 18.

Mpira ulianzia kwa winga hatari zaidi Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, Mganda Brian Majwega ambaye aliukokoto kwa kasi kupitia wingi ya kushoto kisha akapiga krosi iliyonaswa na Yahya ambaye aliukokota mpira kidogo kabla ya kutishia kama anapiga shuti langoni mwa Coastal, lakini akatoa pande kwa Bocco ambaye alifumua shuti kali la mguu wa kulia.

Kipa Fikirini Bakari, ambaye leo alichukua nafasi ya kipa mzoefu Shaban Kado ambaye leo amewekwa kando kutokana na sababu ambazo hazikuwekwa wazi na uongozi wa mabingwa hao wa 1988 wa Tanzania Bara.

Licha ya kucheza vizuri vipindi vyote, Coastal Union FC haikufanikiwa kupata bao kutokana na ugumu wa ngome ya ulinzi ya Azam FC iliyokuwa chini ya Serge Wawa, Aggrey Morris, Shomari Kapombe na baadaye Said Morad, aliyeingia dakika ya 72 kuchukua nafasi ya Wawa aliyeumia nyama za paja.

Kipindi cha pili Azam FC, walitumia mbinu ya kucheza kwa mfumo usioeleweka kwa kubutua butua na kupoteza muda.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Azam FC kutoka Burundi, Didier Kavumbagu, anayeongoza kwa mabao Ligi Kuu kwa sasa akiwa na mabao 10, alionywa kwa kadi ya njano na refa Andrew Shamba kutoka Pwani baada ya kukataa kubadilishwa na Gaudence Mwaikimba katika dakika ya 72 ili kutimiza mbinu za kupoteza muda kulinda bao lao.

Vikosi vilikuwa:
Coastal Union: Fikirini Bakar, Hamis Mbwana, Hamd Juma, Yusuph Chuma, Tumba Lui, Abdallah Mfuko, Joseph Mahundi/ Mkenje Juma dk 61, Hussein Sued, Suleiman Rajabu, Rama Salim na Itubu Imbem/ Lutimba Yayo dk 61  

Azam FC: Aishi Manula, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Aggrey Morris, Serge Wawa/ Said Morad dk. 64, Mudathir Yahaya, Himid Mao, Frank Domayo, Didier Kavumbagu/ Gaudence Mwaikimba dk. 72, John Bocco na Brian Majwega.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video