Na Bertha Lumala, Azam yaing'oa Yanga kileleni
JKT Ruvu na Ndanda FC ni wabababe wa Azam FC. Kwa nini? Hizi ndizo timu pekee zilizofanikiwa kupata ushindi dhidi ya mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.
JKT Ruvu Stars inayonolewa na kocha wa zamani wa Yanga SC, Fred Felix Minziro, ilikuwa timu ya kwanza kuifunga Azam FC baada ya timu hiyo ya wanalambalamba kucheza mechi 38 za Ligi Kuu Tanzania Bara bilka kupoteza mechi hata moja.
VISASI VYALIPWA
Azam inayonolewa na Mganda George 'Best' Nsimbe, aliyechukua mikoba ya Mcameroon Joseph Marius Omog aliyetimuliwa, jana imekamilisha visiasi dhidi ya timu hizo mbili zilizoipiga msimu huu baada ya kuichapa Ndanda FC bao 1-0 katika mechi pekee ya jana ya ligi ya Bara.
Kikosi cha matajiri hao wa Tanzania kilianza kwa kuichapa JKT Ruvu bao 1-0 lililofungwa na Didier Kavumbagu kikiwa nbi kisasi baada ya maafande hao kushinda 1-0 kupitia bao la mshambuliaji aliye katika kiwango cha juu msimu huu, Samwel Kamuntu.
Jana mabingwa hao watetezi wameichapa Ndanda FC 1-0 bao la Mrundi Kavumbagu pia lililomfanya afikishe mabao 10 na kuchekelea kileleni mwa wafumania nyavu msimu huu.
Ushindi huo ambao ni kisasi baada ya Ndanda FC kuichapa Azam FC bao 1-0 katika mechi ya mzunguko wa kwanza mjini Mtwara, umewafanya wanalambalamba wafikishe pointi 33 baada ya mechi 17, pointi mbili mbele ya Yanga SC wanaokamata nafasi ya pili baada ya mechi 16.
Ligi hiyo itaendelea Jumatano Simba SC waliopo nafasi ya tatu ya msimamo wakiwa na pointi 29 baada ya mechi 18, watakapokuwa wageni wa Mgambo Shooting Stars Uwanja wa CCM Mkwakwani jijini Tanga.
0 comments:
Post a Comment