Tuesday, March 24, 2015


Na Bertha Lumala, Tanga
Baada ya timu yake kupokea kipigo chembamba dhidi ya Azam FC, kocha mkuu wa Coastal Union, Mkenya James Nandwa, ameamua kujiuzulu, imefahamika.

Coastal Union, mabingwa wa 1988 wa Tanzania Bara, walipoteza mechi yao ya tano msimu huu baada ya kukubaki kipigo cha bao 1-0 dhidi ya wanalambalamba, Azam FC Uwanja wa Mkwakwani jijini hapa mwishoni mwa wiki iliyopita.

Mara tu baada ya mechi hiyo kumalizika, kumekuwa kukifanyika vikao vya mara kwa mara vya uongozi na benchi la ufundi la Coastal Union, na taarifa za kina kutoka kwenye vikao vivyo zinaeleza kuwa Nandwa ameachia ngazi.

Mtandao huu umefanya mahojiano na Nandwa jijini hapa leo mchana ambapo kocha huyo amesema ameamua kuondoka mwenyewe jijini hapa kutokana na matokeo mabovu ya Coastal tangu alipopewa mikoba ya Mkenya mwenzake, Yusuph Chipo, ambaye hakurejea nchini baada ya mapumziko ya Novemba baada ya kupata timu nyingine ya kuinoa nchini kwao.
 
"Ni kweli tulifanya vikao baada ya mechi na hata leo asubuhi tumeendelea na vikao na uongozi kuzungumzia mechi yetu ya jana (juzi) dhidi ya Azam na hali timu yetu msimu huu," Nandwa amesema.

"Si kwamba nimefukuzwa, nimeamua niondoke mwenyewe kutokana na matokeo mabovu ambayo timu inayapata. Nimezungumza na viongozi, ninaamini muda si mrefu kila kitu kitawekwa wazi. Julio ndiye amepewa timu."

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Coastal Union, amesema uongozi haujamtimua Nandwa bali ameandika barua mwenyewe kuomba kuachia ngazi.

Assenga amesema Julio atasaidiwa na aliyekuwa kocha mkuu wa Africans Sports, Joseph Lazaro.

"Tutamrejesha Lazaro hapa kwa sababu tuliwaazimisha tu Sports ili awasaidie kupanda daraja, hatukuvunja mkataba na Lazaro," amesema Assenga.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video