ATLETICO Madrid ya Hispania imefanikiwa kutinga robo fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya kwa mikwaju ya penalti 3-2 dhidi ya Bayer Leverkusen ya Ujerumani.
Mshindi amelazimika kupatikana kwa mikwaju ya penalti usiku huu kufuatia Atletico kushinda 1-0 katika dakika 120 sawa na Leverkusen walioshinda 1-0 nyumbani kwao ndani ya dakika 90.
Wastani wa mabao ni 1-1 na dakika 30 za nyongeza timu hizo zilitoka 0-0.
0 comments:
Post a Comment