Mabingwa watetezi wa michuano ya
Kombe la FA,washika mitutu wa London Arsenal wanatarajiwa kupambana na Bradford City au Reading
katika hatua ya nusu fainali baada ya kuwatandika Manchester United hapo
jana.
Katika mchezo mwingine wa nusu fainali ya michuano hiyo
Aston Villa wao watakwaana na mshindi kati ya Liverpool au Blackburn
Rovers.
Reading na Bradford zinatarajiwa kucheza mchezo wao wa
marudiano wa robo fainali Machi 16, huku mchezo baina ya Blackburn na
Liverpool ukiwa bado haujathibitishwa siku utakayochezwa.
Mechi za nusu fainali zote zinatarajiwa kuchezwa katika Uwanja wa Wembley April 18 na 19 mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment