Wednesday, March 11, 2015


Na Bertha Lumala, Dar es Salaam 
Beki wa kati George Michael wa Ruvu Shooting Stars ya Pwani ameoneshwa kuwa hakuonewa na TFF kufungiwa mechi tatu baada ya jana kuoneshwa kadi nyekundu uwanjani.

Beki huyo mwenye nguvu nyingi alifungiwa na shirikisho hilo la soka nchini baada ya kupatikana na hatua ya kumkaba koo mshambuliaji na mfungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita, Mrundi Amisi Tambwe wa Yanga SC katika mechi yao iliyomalizika kwa suluhu Uwanja wa Taifa jijini hapa Januari 18 mwaka huu.

Akicheza mechi yake ya kwanza jana baada ya kutumikia adhabu ya kukosa mechi tatu, beki huyo ametolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 75 kutokana na kucheza katika hali ya hatari uwanjani wakati timu yao ikimenyana dhidi ya Polisi Moro FC Uwanja wa Jamhuri mjini Moro.

Masau Bwire, msemaji wa Ruvu Shooting, amesema hawajaridhishwa na uamuzi wa refa kuhusu kadi hiyo, lakini hawana budi kuuheshimu kwani ndiye mwenye uamuzi wa mwisho.

Timu hizo zimetoka suluhu katika mechi hiyo pekee ya leo ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video