Na kosseyi deogaratius;
KIUNGO mpiganaji wa Chelsea Nemanja
Matic aliadhibiwa kukosa mechi tatu kwa kosa la kutaka kulipiza kisasi kufuatia
rafu mbaya aliyochezewa katika pambano lao dhidi ya Burnely.Hata hivyo
alipunguziwa adhabu na kuwa mechi mbili kufuatia klabu yake kukata rufaa.Tayari
amekosa pambano la fainali la Capital One ambapo Chelsea imeweza kutwaa taji
hilo dhidi ya Spurs.Pia atakosa pambano gumu dhidi ya West Ham ambapo Chelsea
inapigana kutanua pengo la pointi 8 dhidi ya Manchester city.
Kwangu mimi adhabu ya Matic ina
faida kubwa mbili kwa Chelsea. Kwanza anapata muda mwingi wa kumpuzika kabla ya
pambano gumu sana la marudiano dhidi ya PSG,lakini pia anahifadhi nguvu zake
ambazo ni muhimu sana kwa timu yake katika kumalizia ligi
Faida nyingine ni kuwa adhabu
yake inamfanya akose mechi,hii ina maana kuwa inamweka kando na uwezekano
mkubwa wa kupata na majeraha.Ikumbukwe kuwa ligi ya wingereza ni ngumu sana
katika mechi za kumalizia hasa kwa timu zinazopigania taji na zile zinazojiokoa
na kushuka daraja.Kwa maana hiyo basi atakaporejea atakuwa na msaada mkubwa kwa
timu yake kumalizia ligi.
Hakuna shaka matic ni mtu muhimu
mno kwa Chelsea.Tazama pambano la chesea kupoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Newcastle
Matic hakuwepo uwanjani.Pia kipigo cha mabao 5-3 kutoka kwa Spurs Matic
hakuwepo uwanjani,hata ile sare ya 1-1 dhidi ya Burnely ilikuja mara baada
ya Matic kutolewa kwa kadi nyekundu.Hata
pambano la fainali ya capital one japokuwa Chelsea ilifanikiwa kushinda lakini
ilizidiwa mno na Spurs kwenye eneo la kiungo.Nacer Chadli,Nadeer Bentaleb na
Lee Mason waliitawala Chelsea katika kiungo.
Haina ubishi Matic ni muhimili
mkubwa kwa Chelsea.Uwepo wake uwanjani unaifanya Chelsea iwe na uwiano wa
kushambulia na kuzuia.Timu nzima inacheza kwa uhuru.Eden Hazard,Willian na
Fabrigas wanakuwa na jeuri ya kushambulia kwakuwa wanajua nyuma kuna mtu
anaelinda timu.Safu ya ulinzi inakuwa na utulivu mkubwa kwasababu mbele yake
kuna Matic.Kama ilivyo kwa Yaya Toure kwa Man city ndivyo ilivyo kwa Matic kwa
Chelsea.Matic anatoa kila kitu kwa timu.Anakaba,anatuliza timu,anaendesha timu
lakini pia anashambulia.Kubwa zaidi matic
ni mpambanaji mkubwa asiye choka.
0 comments:
Post a Comment