KUNDI LA Yanga katika mtandao wa kijamii wa facebook Yanga facebook Familiy limetoa pongeza kwa timu yao hususani kocha mkuu, Hans van der Pluijm baada ya jana usiku kuwaondoa mashindano BDF XI.
Yanga walifungwa mabao 2-1 katika uwanja wa Lobatse mjini Gaborone, lakini wamesonga mbele kutokana na ushindi wa maba0 2-0 waliyopata Dar es salaam katika mechi ya kwanza ya kombe la shirikisho.
"Well done super coach Hans van der Pluijm.Yanga facebook family inawapongeza beach la ufundi na viongozi wote waliongozana na timu yetu bila kumsahau Mlezi wetu Yusuphed Mhandeni na Kamanda Jerry Muro hongereni sana tulitamani wote tuhuzurie lkn imeshindikana lkn Mungu kawajibu wote waliohusika na huu udhwalimu."
Wakati huo huo, Msemaji wa Ruvu Shootings, Masau Bwire ameonesha uungwana baada ya kutoa maneno ya pongezi kwa Yanga kufanikiwa kusonga mbele.
"Hongereni sana Jangwani kwa kufuzu kuingia hatua nyingine. Msibweteke, anzeni maandalizi ya hatua inayofuata ili pia mfanye vizuri. Shooting tupo Mbeya, tunatonesha kidonda
mlichowatia hawa jamaa wa City! Leo huenda watamfukuza kocha" Ameandika Masau katika akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa facebook.
mlichowatia hawa jamaa wa City! Leo huenda watamfukuza kocha" Ameandika Masau katika akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa facebook.
0 comments:
Post a Comment