Wachezaji wa Yanga wakifanya mazoezi leo
WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya kombe la Shirikisho, Dar Young Africans wameendelea na mazoezi ya mwisho mwisho nchini Botswana kujiandaa na mchezo wa marudiano dhidi ya wenyeji BDF XI itayopigwa kesho ijumaa, februari 27 mwaka huu.
Yanga chini ya kocha mkuu, Mholanzi, Hans van der Pluijm wapo katika morali ya ushindi na wachezaji wote waliosafiri wapo salama ambapo leo wamefanya mazoezi vizuri kabisa.
Bahati nzuri kwa Yanga ni kwamba wataingia uwanjani wakiwa na faida ya mabao 2-0 waliyovuna uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, februari 14 mwaka huu.
Mabao yote mawili siku hiyo yalifungwa na Mrundi, Amissi Joselyn Tambwe.
Ili kusonga mbele Yanga wanahitaji ushindi, suluhu au sare ya aina yoyote ile au wasifungwe zaidi ya goli 1-0.
Habari njema kwa wapenzi wa soka nchini ni kwamba mtanange huo utaoneshwa moja kwa moja 'Live' kipitia kituo cha Televisheni cha Azam TV kuanzia majira ya saa 2:30 usiku.
Mechi ya kwanza Dar es salaam, Yanga walipiga marufuku chombo chochote cha TV kuonesha mechi hiyo, lakini safari hii matangazo yatapokelewa na Azam TV moja kwa moja kutoka Botswana na kuwafikia Watanzania wote.
Kocha mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm (kushoto) baada ya mazoezi akiwa ameketi na nahodha Nadir Haroub 'Cannavaro' kwenye basi walilotumia kutoka Hotelini kwenda uwanjani.
0 comments:
Post a Comment