LEO mchana Yanga wamegoma kula chakula cha mchana walichoandaliwa katika hoteli waliyofikia mjini Gaborone kwa lengo la kulinda afya za wachezaji wao.
"Kikubwa zaidi tulichojifunza katika safari yetu ya Botswana ni kuwashirikisha Watanzania wanaoishi katika nchi ambazo tunashiriki michuano kwasababu tumepata ushirikiano kikamilifu kutoka kwa Watanzania wa hapa. Licha ya wengine kuwa wapinzani kwa kule nyumbani, hapa wametuunga mkono. Tuliamua kutokula chakula wa mchana katika hoteli yetu tofauti na siku za nyuma tangu tumefika kwasababu ya kulinda afya za wachezaji.
Hwa Wabotswana wamejitahidi sana kuhakikisha wanajaribu kutushinda nje ya uwanja. Kwa asilimia 100 tumepambana na tuko sawa kimchezo. Niwaambie Watanzania wote wazidi kutombea, yaani timu zote za Tanzania katika michuano ya kimataifa." Amesema makamu mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga kutoka mjini Gaborone, nchini Botswana.
Mechi ya BDF XI na Yanga inaanza majira ya saa 2:00 usiku huu, Yanga wakihitaji sare ya aina yoyote ile au kutofungwa zaidi ya goli 1-0 kwani mechi ya kwanza walishinda 2-0.
0 comments:
Post a Comment