Monday, February 2, 2015


Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
Baada ya kuambulia pointi tatu katika mechi tatu zilizopita Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Yanga imetua jijini Tanga ikiwa na kikosi chenye nyota wake wote 24 tayari kusaka ushindi wa kupoza uchungu dhidi ya Coastal Union kesho.

Yanga SC imeambulia sare katika mechi zote tatu zilizopita kwenye uwanja wake wa nyumbani ikitoka 2-2 dhidi ya Azam FC, 0-0 dhidi ya Ruvu Shooting kabla ya jana kuuanza vibaya mwezi Februari kwa kutoka suluhu dhidi ya kikosi chenye wachezaji 10 cha Ndanda FC kilichokuwa kinacheza kwa mara ya kwanza Uwanja wa Taifa tangu kipande daraja msimu huu.

Timu hiyo ya Jangwani itakuwa na kibarua kigumu mbele ya kikosi cha kocha mkuu mpya Mkenya James Nandwa cha Coastal Union watakapopambana katika mechi ya kiporo ya raundi ya 10 ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga Jumatano.

Mechi hiyo Na. 66 ilipaswa kuchezwa Januari 10 lakini ikapigwa kalenda na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutokana na ushiriki wa Yanga katika michuano ya Kombe la Mapinduzi 2015 kilikotolewa hatua ya robo fainali dhidi ya JKU ya Unguja.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za makao makuu ya Yanga zilizopo makutano ya mitaa ya Jangwani na Twiga jijini Dar es Salaam leo asubuhi kabla ya kuanza safari ya kwenda Tanga, Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema: "Inauma kupata matokeo ya sare nyumbani dhidi ya timu ndogo kama Ndanda FC."

Raia huyo wa Uholanzi amesema timu yake inakabiliwa na changamoto ya kukosa umakini katika umaliziaji, jambo ambalo amesema linamshangaza kwani washambuliaji wake wamekuwa wakitupia mara kwa mara mazoezi lakini hawafanyi kweli wanapocheza dhidi ya timu pinzani.

"Kila mmoja wetu ndani ya kikosi ameumizwa na matokeo ya sare dhidi ya Ndanda FC, tulicheza ovyo sana kipindi cha kwanza, kipindi cha pili tulibadilika, pengine kutokana na maneno ambayo tuliwaambia wachezaji wakati wa mapumziko.

"Lakini bado tulikosa mabao mengi na mwisho tukatoka sare nyumbani. Tunakwenda Tanga leo na wachezaji wote, hata waliokuwa wagonjwa na majeruhi; (Mbuyu) Twite, (Haroun) Niyonzma na (Deogratius Munishi) Dida tunakwenda nao kusaka ushindi ili turejeshe matumaini yetu ya kupigania ubingwa," amesema zaidi kocha huyo.

Tangu arejee Yanga SC Desemba mwaka jana kurithi mikoba ya Mbrazil Marcio Maximo aliyetimuliwa, Pluijm ameiongoza timu hiyo ya Jangwani katika mechi nane (nne za VPL na nne za Kombe la Mapinduzi) akishinda nne (moja tu ya VPL), sare tatu na kupoteza moja.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mwasiliano wa Yanga, Jerry Muro aliyefuatana na kikosi cha Yanga jijini Tanga, amesema kuwa leo mchana wamefungua tawi jipya na kuzungumza na wanachama wao wa Handeni kabla ya kuingia mjini Tanga.

Muro amesema kikosi chao kesho kitafanya mazoezi asubuhi na jioni mjini Tanga, tayari kumenyana na mabingwa hao wa Tanzania Bara 1988, Coastal Union ambao msimu huu wamepoteza mechi moja tu kwenye uwanja wao wa nyumbani.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video