Tuesday, February 3, 2015


Na Bertha Lumala, Tanga

Mabingwa mara 24 wa Tanzania Bara, Yanga SC wamekataa hoteli zilizokuwa zimeandaliwa na wenyeji wao Coastal Union jijini Tanga huku wakiagiza Uwanja wa CCM Mkwakwani ulindwe muda wote kuzuia ushirikina.

Kikosi cha Yanga SC kimeingia jijini hapa leo alasiri kikitokea Dar es Salaam kikiwa na mabasi mawili makubwa na mara tu baada ya kuwasili, baadhi ya watu wake walikwenda moja kwa moja kwenye Uwanja wa CCM Mkwakwani na kumwambia Meneja wa uwanja huo Mbwana Msumari ahakikishe uwanja unalindwa muda wote.

Waandishi wa habari waliokwenda kwenye Uwanja wa CCM Mkwakwani leo asubuhi kuangalia mazoezi ya Yanga SC, hawakuikuta timu hiyo uwanjani hapo badala yake walikuta mabaunsa wakiulinda.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga, Jerry Muro, amesema: "Tuna utaratibu maalum wa kuweka timu hotelini, hatuwezi kukubali kuandaliwa hoteli na Coastal Union. Watu wetu wa sekretarieti walitangulia mapema kuja kuandaa hoteli hapa."

COASTAL WATANGZA VITA
Kwa upande wao Coastal Union wametangaza vita ya dakika 90 dhidi ya Yanga katika mechi hiyo pekee ya kesho ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Oscar Assenga, msemaji wa Coastal Union, amesema kikosi chao kiko tayari kuchukua pointi tatu dhidi ya Yanga kesho.

"Tumefanyia kazi upungufu uliojitokeza katika mechi mbili zilizopita dhidi ya Polisi Moro na Mtibwa Sugar, timu kwa sasa iko vizuri na tunatangaza rasmi vita ya uwanjani kati yetu na Yanga kesho. 

"Tunaomba mashabiki wetu wasifanye vurugu kwa kurusha chupa uwanjani kama ilivyotugharimu mwaka jana kwa kupigwa faini na (Shirikisho la Soka Tanzania) TFF.

"Kocha Mkuu (Mkenya James Nandwa) amekiongoza kikosi katika mazoezi ya mwisho leo kuanzia saa 1:00 hadi saa 2:45 asubuhi. Jioni tunapumzika kusubiri muda wa kuinyoa Yanga ufike," amesema zaidi Assenga.

YANGA SC NAO WASEMA WATASHINDA
"Wachezaji wote wa Yanga msimu huu wako 'fiti' isipokuwa Dida ambaye tumemwacha Dar es Salaam kwa sababu hajapona malaria. Tuko Tanga kwa lengo la kuwapa raha mashabiki wetu kwa kushinda mechi," amesema Muro.


Coastal chini ya kocha mkuu mpya, Nandwa, inatamba na mshambuliaji wake mpya Mkenya Rama Salim ambaye amefunga mabao manne msimu huu, moja nyuma ya kinara wa mabao Yanga msimu huu, winga mzawa Simon Msuva. 

Mashabiki wa timu hizo wamekuwa na uhasama mkubwa kutokana na upinzani uliopo kati ya timu zao. Agosti 24, 2013 basi la wachezaji wa Coastal Union lilishambuliwa kwa mawe na mashabiki waliodaiwa kuwa wa Yanga muda mfupi baada ya mechi yao kwanza ya VPL kumalizika kwa sare ya bao moja kwenye Uwanja wa Taifa.

Mashabiki wa Yanga walifura kwa hasira kutokana na wageni wao kupewa penalti dakika ya mwisho na refa bora wa VPL msimu wa 2011/12, Martin Saanya wa Morogoro.

Penalti hiyo ilimsababisha refa huyo kufungiwa msimu mzima na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kabla ya kuokolewa na msamaha wa Rais wa shirikisho hilo, Jamal Malinzi kwa wafungwa wote wa TFF alioutoa usiku wa kuamkia Oktoba 28, 2013, muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi wa kiti hicho katika uchaguzi mkuu uliopita.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video