KLABU ya Yanga kupitia Mwenyekiti wake Yusuf Manji
imewasilisha pendekezo mbele ya Marais wanaounda Umoja wa Afrika (AU) kuanzisha
mashindano maalum ya kupambana na ugonjwa wa Ebola lakini kwa kuanzia akatoa
kiasi cha Dola 500,000 kwa kuanzia.
Pendekezo hilo la Manji amelitoa Alhamisi ya
Januari 29 wiki iliyopita jijini Adis Ababa nchini Ethiopia kulikofanyika
mkutano huo ambao kwa nchi uliwakilishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dk Jakaya Kikwete huku Manji akiwa mmoja wa wageni.
Akizungumza na waandishi wa habari leo mchana
Katibu wa Yanga Jonas Dk Tibohora ambaye naye aliongozana na Manji alisema
katika kikao hicho cha 24 cha AU Manji amewasilisha pendekezo hilo akitaka nchi
54 za Afrika kushiriki katika mashindano hayo mafupi kusaka fedha za kupambana
na ugonjwa huo hatari unaiosumbua Afrika Magharibi kwa kuchukua washindi wawili
wa juu katika kila ligi.
Tibohora amesema katika pendekezo hilo la Manji
ambalo nchi zote zililiafiki Manji ametaka mashindano hayo kuchezwa kwa kanda
za nchi huzika ambapo mechi hizo zitachezwa kwa mfumo wa nyumbani na ugenini
huku kila klabu ikitakiwa kuchangia kiasi cha dola 100000 (shilingi mil 170)
kama kiingilio.
Amesema lengo la Manji ni kutaka kuona soka
linachangia katika mapambano ya ugonjwa huo ambapo jumla ya kiasi cha dola 10.8
ml zitaweza kupatikana huku mwenyekiti huyo akitangulia kutoa dola 500000 kama
kianzio.
"Mwenyekiti amependekeza kwamba kwa kuwa
Yanga tunaitwa Young African Football Club jina letu lifanye kitu kuhusu Afrika
na kwa kuwa kila kanda za afrika mfano hii ya kwetu ya Afrika Mashariki tuna
utaratibu wetu wa kumaliza msimu mashindano hayo sasa yafanyike kwa kanda ili
kuweza kupatikana muda mzuri wa kuchezeka mechi hizo,"alielezea Tibohora.
"Kwa kuwa mechi hizo zitakuwa zikiendeshwa
kwa mfumo wa nyumbani na ugenini Manji ameomba klabu itakayocheza nyumbani itoe
nusu ya mapato ya kwenye mechi husika iende katika mapambano hayo hapo pia
klabu zitanufaika na nusu ya mapato hayo lakini pia ushindani huo utazinufaisha
baadhi ya nchi."
0 comments:
Post a Comment