MECHI ya marudiano ya kombe la Shirikisho baina ya wenyeji BDF XI ya Botswana dhidi ya Yanga ya Dar es salaam litaanza saa 2:00 usiku kwa saa za Afrika mashariki.
Saa za Botswana itakuwa saa 1:00 usiku.
Awali ilitangazwa kuwa mchezo huo ungeanza saa 12:00 jioni hii, lakini kulikuwa na mkanganyiko wa muda na taarifa rasmi ni kwamba saa mbili usiku ndio kituo cha matangazo cha Azam TV kupitia chaneli ya Azam TWO kitakuletea maelezo ya moja kwa moja kutoka Gaborone, Botswana.
Yanga wanahitaji sare ya aina yoyote ile au kutofungwa zaidi ya goli 1-0 ili kusonga mbele.
Hii inatokana na ushindi wa 2-0 walioupata Dar es salaam, februari 14 mwaka huu uwaja wa Taifa.
0 comments:
Post a Comment