VIGOGO wa England Manchester United, Liverpool, Everton,
Tottenham wamechomoza na ushindi wa kuvutia na kuungana na timu za Newcastle
United, Stoke City na Sunderland kutengeza ‘ Jumamosi isiyo na sare’. Wakati
Chelsea itashuka Stamford Bridge kuwakabili mabingwa watetezi Manchester City
ayari michezo saba imepigwa na yote imetoa washindi.
Katika mechi ya mapema, Newcastle ilichomoza na ushinsi wa
mabao 3-0 katika uwanja wa The Kingstone Communications dhidi ya wenyeji Hull
City. Remy Cabella alifunga bao la kuongoza kwa wageni dakika tano kabla ya
kumalizika kwa kipindi cha kwanza, Sammy Ameobi akafunga lingine dakika tano
baada ya kuanza kwa kipindi cha pili, kabla ya
Yoan Gouffran kuitmishushindi wa ‘ The Toon’.
Bao pekee kunako
dakika ya pili lililofungwa na Romelo Lukaku lilitosha kuwapa ushindi wa kwanza
‘ Toffie’ baada ya michezo tisa. IKicheza uwanja wa nyumbani Selhurs Park,
Crystal Palace ilishuhudia ikikubali kichapo cha goli 1-0 kutoka kwa vijana hao
wa Roberto Martinez, hiko ni kipigo cha kwanza kwa mkufunzi wa Palace, Alan
Pardew.
Kijana anayeibeba Liverpool hivii sasa, Rahem
Sterling aliwafungia ‘ Majogoo wa Anfield’ bao la kuongoza katika dakika
ya 51 wakatI timu yake ya Liverpool ilipowashinda ‘ Wagonga nyundo wa London’
West Ham United kwa mabao 2-0. Mshambulizi Daniel Sturridge aliingia kuchukua
nafasi ya Lazar Markovic katika dakika ya 68 na kucheza kwa mara ya kwanza
baada ya kuwa nje kwa miezi mitatu. Mshambulizi huyo wa England aliwafungia
Liverpool bao la pili zikiwa zimesalia dakika kumi mchezo kumalizika katika
uwanja wa Anfield.
Manchester United imefanikiwa kulipa kisasi dhidi ya
Leicester City kufuatia kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 katika uwanja wa Old
Trafford. Robbin Van Persie na Radamel Falcao walifunga katika dakika za 27 na
32 kabla ya Wes Morgan kujifunga dakika ya 44 na kufanya vijana wa Luis Van
Gaal kuwa mbele kwa mabao 3-0 kufikia nusu ya mchezo. Marcin Wasilewski
aliwafungia wageni bao la kufutia machozi katika dakika ya mwisho ya mchezo.
Ikicheza katika uwanja wa nyumbani, Britania, Stoke City
iliichapa QPR kwa mabao 3-1. Jonathan Walters alifunga mara mbili katika dakika
za 21 na 24 kabla ya Niko Kranjcar
kuiwafungia wageni goli la kufutia machozi katika dakika ya 36. Walters
alifunga ‘ hat-trick’ baada ya kuzamisha bao la tatu dakika ya mwisho ya
mchezo.
Mshambulizi Jermaine
Defoe alifunga bao lake la kwanza tangu alipojiunga na Sunderland akitokea
Toronto ya Marekani. ‘ Black Cats’ walichomoza na ushindi wa mabao 2-0 katika
uwanja wa Stadium of Right dhidi ya
Burnley. Connor Wickham aliwafungia wenyeji bao la kuongoza dakika ya 20
kabla ya Defoe kufunga lingine dakika 14 baadae.
IKicheza katika uwanja wa nyumbani The Hawthorns timu ya
West Brom ilivurumishwa mabao 3-0 na Tottenham Hotspur. Cristian Eriksen aliifungia Spurs bao la
uongozi dakika ya 6 kabla ya Harry Kane kufunga mara mbili katika dakika za 15
na 64 alipofunga kwa mkwaju wa penalti.
Mchezo kati ya Chelsea na City ulimalizika kwa sare ya
kufungana bao 1-1, Loic Remy alitangulia kuwafungia wenyeji dakika ya 41 lakini
kiungo msambulizi, David Silva akaisawazishia timu yake dakika ya mwisho
kuelekea nusu ya kwanza ya mchezo huo .
0 comments:
Post a Comment