Monday, February 2, 2015

Na Omary Sadick

Ni takribani miezi nane imepita toka kumalizika kwa michuano mikubwa duniani katika tasinia ya mpira wa miguu. Michuano hii inajulikana kama kombe la dunia ambapo takribani timu 32 huchuana kuwania kombe hilo mara baada ya kufanyika kwa mchujo kupata timu 5 bora kutoka kwa wanachama wa FIFA ambapo michezo hii huchezwa kwa kuhusisha timu za taifa zinazopatikana katika bara husika.

Katika michuano hiyo ya 20 iliyofanyika nchini Brazil mwezi julai mwaka 2014 toka ilipoanzishwa mnamo mwaka 1930 ilikuwa na historia yake. Mbali nakushuhudia kuanzishwa kwa (goal-line technology) njia ya kuamua kuwa ni goli au sio goli kwa njia ya teknolojia. Jumla ya camera 14 zenye kasi huwekwa na kila goli huwa na camera 7 huku refa huwekewa kifaa katika saa yake ambcaho hutoa mlio wa vibration (kutetemeka) kuashiria kuwa ni goli.

Tukio ambalo lililobeba hisia za watu wengi katika michuano hii ni lile la wenyeji timu ya taifa ya Brazili kufungwa goli 7-1 na timu ya taifa ya ujerumani. Ni tukio ambalo lilileta huzini kwa mashabiki, wapenzi wa timu ya taifa ya brazil. Nikiwa kama kijana ninayefuatilia mpira nilibaki najiuliza imekuaje ila jibu lilibaki kuwa kosa moja goli moja, nidhamu, kujituma ,Ujerumani walikuwa bora kwa kila idara huku Brazil ikiyumba katika nafasi ya kati, nyuma na hata mbele alipokuwa anacheza Fred.

Mchambuzi mmoja wa masuala ya mpira kutoka shirika la utangazaji la BBC bwana Alan Hansen alisema “ katika miaka yake 22 ya uchambuzi wa mpira na katika miaka yake 40 katika michezo hakuwahi kuona kitu kama hicho”

Mwaka 1974 mara baada ya kutwaa taji la mataifa huru barani Africa huko nchini Misri kwa kuifunga timu ya taifa ya Zambia jumla ya goli 4 -2 kufuatia kutoka sare ya 2-2 na mchezo kurudiwa siku mbili baadaye na timu ya taifa ya DR Congo wakati huo ikijulikana kama Zaire kushinda goli 2-0 huku kiungo wake matata wakati huo Mulamba Ndiye akiibuka mfungaji bora kwa kutikisa nyavu mara 9.

Mara baada ya ushindi huo, DR Congo zamani kama Zaire ilienda kushiriki michuano ya kombe la dunia iliyofanyika huko Ujerumani magharibi na hivyo kuwa timu ya kwanza kutoka nchi za chini ya jangwa la sahara na barani Afrika kwa ujmla kushiriki michuano hiyo.

Wakati huo Zaire ilikuwa chini ya utawala wa Mabutu Sese Seko, ambaye alichangia kwa kiasi flani katika mafanikio ya timu ya taifa ya mpira japokuwa wachambuzi wa masuala ya mpira hawakufurahishwa na baadhi ya vitendo alivyofanya mathalani kukifanya chama cha soka cha Zaire kuwa chake, mbali na hilo kuifanya timu ya taifa kuwa kama yake , kubadili jina kutoka samba (lions) na kuita leopard, hata mashabiki hawakuruhusiwa kuonana na wachezaji wao walipokuwa wakirudi toka mashindanoni.


Katika michuano hiyo iliyofanyika huko Ujerumani Magharibi, timu ya taifa ya Zaire ilikuwa kundi moja na timu za taifa za Brazil, Scotland, pamoja na Yugoslavia iliyokuwa ikiundwa na nchi za Serbia, Crotia, Slovenia na Macedonian.


Pamoja na historia hii ya pekee kwa kuwa timu ya kwanza toka Africa kushiriki fainali hizi, tukio ambalo wananchi, mashabiki wa timu ya taifa ya DR Congo (Zaire) hawatalisahau ni hili la kufungwa goli 9 kwa 0 na timu ya taifa ya Yugoslavia.


Katika mahojiano ya shirika la utangazaji la BBC, mchezaji Mwepu Ilunga aliyecheza nafasi ya ulinzi alinukuliwa akisema, kilichowafanya wapoteze mchezo wao dhidi ya Yugoslavia kwa kufungwa goli 9-0, walisikia kuwa hawatalipwa posho zao.

Anasema,“ kabla ya mchezo wetu dhidi ya Yugloslavia, tulifahamu kuwa hatutalipwa pesa zetu, hivyo tukakataa kucheza.” baadaye waliingia uwanjani lakini walicheza pasipo kujituma


Timu ya taifa ya Zaire iliondolewa kwenye mashindano hayo pasipo kufunga hata goli moja, huku yenyewe ikiambulia kufungwa goli 14 katika michezo yake mitatu iliyocheza.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video