Muziki wa Ruvu Shootings kumuulize Amissi Tambwe wa Yanga?
MAAFANDE wa Ruvu Shootings wametamba kuendeleza
dozi katika mechi za ligi kuu Tanzania bara.
Tambo hizo zimekuja siku chache baada ya Maafande
hao wa Mabatini Mlanndizi, Mkoani Pwani kuibuka na ushindi mara mbili uwanja wa
nyumbani, mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar na 2-1 dhidi ya Stand United
Afisa habari wa klabu hiyo, Masau Bwire amesema
kwasasa wapo relini na hakuna wa kuwaondoa, hivyo maafande wa Tanzania Prisons
wajiandae kunyolewa mwishoni wa wiki katika mechi ya ligi kuu itayopigwa uwanja
wa Sokoine jijini Mbeya.
“Hali ya hewa ya Mbeya ni tofauti na Mlandizi,
tunalazimika kuwaleta vijana mapema ili kuzoea hali ya baridi ya Mbeya. Tunataka
wachezaji wasiwe na shida ya kutandaza soka, tunatarajia kuondoka wachezaji 21
na viongozi saba, tutaondoka alhamisi”. Amesema Masau.
“Kocha Mkenya, Tom Alex Olaba ana uhakika na
kikosi chake, amebaini nini kifanyike na tunaamini tutachukua ushindi jumamosi
dhidi ya Tanzania. Ametamba Bwire na kuongeza: “Treini ikiwa kwenye reli huwezi
kuiondoa, tuko kwenye reli, hakuna anayeweza kutuondoa”.
0 comments:
Post a Comment