
TIMU za African Sports ya Tanga na Mwadui FC ya
Shinyanga zinatrajiwa kucheza mchezo wa fainali ya kusaka Bingwa wa Ligi Daraja
la Kwanza (FDL) siku ya jumamosi katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
African Sports waliibuka washindi wa kwanza
katika Kundi A, na Mwadui FC washindi wa kwanza Kundi B watacheza mchezo huo wa
fainali ambapo Bingwa atapewa zawadi ya Kombe na medali, hali kadhalika kwa
msindi wa pili.
Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ilimalizika
mwishoni mwa wiki kwa timu nne kupanda Ligi Kuu kwa kila kundi kutoa timu
mbili, Kundi A ni African Sports na Majimaji FC, Kundi B ni timu za Mwadui FC
na Toto Africans.
Baada ya kupokea taarifa hizo, kocha mkuu wa
Mwadui FC, Jamhuri Kwhelo ‘Julio’ ametamba kushinda mechi hiyo na kuwadhihirishia
Watanzania kuwa yeye ni miongoni mwa makocha bora nchini.
“Kwanza namshukuru
Mungu mwingi wa rehema kwa kutuwezesha kucheza tena ligi kuu ya Vodacom,
kumbuka mwaka jana tulipanda na kupata nafasi hiyo, lakini hatukuweza kucheza”.
Amesema Julio na kuongeza : “ Mwaka huu tulijipanga upya na kuanza mchakato na
hatima yake tumeweza kumaliza tena kwa kwanza katika kundi letu”.
Kuhusu mechi ya jumamosi, Julio amesema: “Tumepata
taarifa kuwa tutacheza mchezo wa kutafuta bingwa wa jumla wa ligi daraja la
kwanza, kwetu sisi tuko tayari na timu yangu inaondoka kwa basi maalumu kuja
kucheza mechi hiyo siku ya jumamosi”.
“Tunataka kushinda mechi hiyo ili watu wajue kuwa
Julio ni moja ya makocha bora nchini”
0 comments:
Post a Comment