Na Amplifaya Amplifaya
KOCHA wa timu ya Taifa ya Kuogelea, AlexMwaipasi amesema Tanzania inatarajiwa kushiriki kwenye mashindano ya Kanda ya Nne yaliyopangwa kufanyika nchini Angola, Mei mwaka huu.
Mara ya mwisho mashindano hayo kufanyika ilikuwa ni mwaka jana nchini Uganda ambapo Tanzania iliwakilishwa na wachezaji kadhaa waliofanya vizuri wakiwamo Hilal Hilal na Sonia Tomiotto.
Akizungumza jana, Mwaipasi alisema katika kuhakikisha wanafanya vizuri katika mashindano ya mwaka huu, tayari
wameshaanza mchakato wa kusaka kikosi bora.
“Tumeanza mchakato wa kuwatafuta wachezaji
bora kutoka mikoa ya Mwanza, Arusha,
Morogoro na Dar es Salaam na tuna imani
mambo yatakuwa mazuri tutakapoanza kambi
baadaye,” alisema Mwaipasi.
Alisema wachezaji hao watafuatiliwa mwenendo
wao katika mashindano ya kitaifa
yatakayofanyika mwezi ujao, na mashindano ya
wazi ya Afrika yatakayofanyika nchini Afrika
Kusini.
0 comments:
Post a Comment