
KOCHA mkuu wa mabingwa wa zamani wa Tanzania mwaka
1988 waliofanikiwa kurejea tena ligi kuu soka Tanzania bara, Africans Sports ya Tanga, Joseph Lazaro
amefichua siri ya kapata mafanikio katika michuano ya ligi daraja ya kwanza
iliyomalizika mwishoni mwa wiki iliyopita.
Africans Sports walimaliza vinara wa kundi A
wakati Mwadui fc walimaliza wa kwanza kundi B, na timu hizo zitachuana jumamosi
ya wiki hii uwanja wa Taifa, Dar es salaam kutafuta bingwa wa jumla wa ligi
daraja la kwanza.
Akizungumza na mtandao huu, Lazaro amesema: “Siri
ya kufanya vizuri kwangu ni kuwa karibu mno na wachezaji, kitu cha pili ni kujua
malengo yetu. Wachezaji wangu na viongozi wangu tulikuwa na lengo la kupanda
daraja”.
“Wachezaji ndio watakaokuangusha au kukubeba,
lazima uwe karibu nao. Hivi nipo mazoezini, nakuja huko Dar es salaam, mimi
naona kama ligi haijaisha. Nataka Nafasi ya kuwa bingwa wa makundi yote mawili”.
0 comments:
Post a Comment