SIMBA inaanza mazoezi leo jioni jijini Tanga kujiandaa na mechi ya keshokutwa dhidi ya Coastal Union itakayopigwa uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga.
Afisa habari wa klabu hiyo, Humphrey Nyasio amezungumza na mtandao huu na kueleza kuwa kikosi kipo salama na wapo tayari kwa mechi hiyo.
Nyasio amefurahishwa na jinsi mashabiki walivyowapokea kwa furaha jijini Tanga na wamejipanga kuwapa furaha zaidi kwa kushinda kipute hicho.
Hata hivyo, Afisa habari huyo ameongeza kuwa beki wa kati Joesph Owino amebaki Dar es salaam akiendelea kufanya mazoezi mepesi na kikosi cha Simba B.
0 comments:
Post a Comment