“Niwaambie ukweli mashabiki wangu, kila mtu
anayeniunga mkono ni kama familia yangu, kila shabiki wangu ni kama mtoto
wangu, kila shabiki ni mtu muhimu kwangu, kila shabiki ni muhimu kwa Simba,
lakini kila shabiki lazima aelewe kitu hiki muhimu;
“Timu hii ni changa sana, timu hii inahitaji muda,
sisemi kuwa tunahitaji miaka kumi, hapana! Tunahitaji muda, nilikuja
nimechelewa, nikiwa na Matola tunajaribu sana kuiboresha timu hii, lakini timu
hii ina presha, tunawapa presha kubwa wachezaji wangu kila wiki, lakini
wachezaji wangu hawana uzoefu kwasababu ni wachanga”
Wakati fulani tunacheza vizuri, wakati fulani
tunaanguka, wakati fulani tunashinda, kila shabiki lazima aelewe kitu hiki,
hata sare, lazima wawape wachezaji wangu nguvu kwa ajili ya mechi ijayo,
unapoanza kupiga kelele..aaaah! nini? Aaaah! mechi inayofuata inakuwa hatari
zaidi kwa mchezaji mchanga kwasababu hana uzoefu wa kuwaza mechi iliyopita, pia
hana uwezo binafsi wa kujijenga na kuongeza morali ya mchezo ujao”.
“Kwa timu yangu, kocha Goran anaahidi, kila mechi,
kila mazoezi, ninafanya kazi kwa asilimia mia moja, wachezaji wangu kila
wanapocheza mechi wanacheza kwa juhudi, wanacheza kwa ajili ya Simba, lakini
wakati fulani hatushindi kila mechi”
Maneno haya yamezungumzwa na kocha mkuu wa Simba Sc, Goran Kopunovic wakati huu kikosi chake kikijiandaa kuivaa Prisons uwanja wa Taifa, Dar es salaam katika mechi ya ligi kuu Tanzania bara.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, Simba walifungwa bao 1-0 dhidi ya Stand United katika mechi ya ligi kuu iliyopigwa uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga.
0 comments:
Post a Comment