Friday, February 27, 2015


SIMBA SC imemaliza mazoezi yake ya mwisho jioni hii uwanja wa JKT Mbweni Dar es salaam wakijiandaa na mechi ya kesho ya ligi kuu soka Tanzania bara itayopigwa kesho jioni uwanja wa Taifa Dar es salaam dhidi ya Tanzania Prisons.
Kocha mkuu wa Simba, Goran Kopunovic ana matumaini ya kufanya vizuri kesho akidai maandalizi waliyoyafanya toka wafungwe 1-0 na Stand United wiki iliyopita yanatosha kuwapa pointi tatu muhimu.
"Mechi haitakuwa rahisi, timu zinaikamia Simba. Mimi na msaidizi wangu Matola tunafanya kazi kwa asilimia 100 kuiboresha timu. Kwa bahati mbaya wachezaji wangu wengi ni wachanga. Mechi na Prisons tuko tayari na tunarajia kushinda kutokana na mazoezi tuliyoyafanya". Goran amezungumza na mtandao huu jioni hii.
Kesho wachezaji wa Simba watanyosha misuli kidogo kabla ya kuondoka mchana kwenda uwanjani.
Simba imeweka kambi Hoteli ya Ndege Beach iliyopo kambi ya Jeshi ya JKT Mbweni.
Kwa sasa Simba wanashika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi kuu wakijikusanyia pointi 20 baada ya kucheza mechi 15.
Wameshinda mechi 4, sare 8 na kufungwa 3. Wamefunga magoli 15 na kufungwa 12, tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa ni 3.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video