Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam,
Niliuponda sana usajili wa Simba SC
wakati wa majira ya usajili katikati ya mwaka uliopita, nilikosoa namna '
kamati ya usajili' chini ya Zacharia Hans Poppe ilivyokuwa inafanya kazi yake '
kiholela', Poppe kama mkuu wa kamati hiyo alishindwa kabisa kutekeleza mahitaji
ya mwalimu Z.Logarusic ambaye alipendekeza wachezaji kadhaa kutemwa na wengine
kusajili. Nakumbuka, LOGA alipendekeza majina ya wachezaji 15 wa kuachwa huku
akisema kuwa 'hawana hadhi ya kuichezea klabu hiyo kubwa na yenye histori ya
kuvutia' Tanzania na ukanda wa Afrika Mashariki na Kati. Edward Christopher,
Henry Joseph, Zahoro Pazzi, Mkenya, Donald Mosoti, Mrundi, Gilbert Kaze, ni
baadhi ya wachezaji waliondoka klabuni hapo kwa sababu tofauti, kumalizika kwa
mikataba, kushuka kwa viwango na mambo ya kinadhamu yalichangia kuwaondoa
mastaa ili kupisha ujenzi wa timu hiyo katika timu hiyo ambayo inasotea nafasi
mbili za juu katika ligi kuu Bara kwa msimu wa tatu sasa.
" Usajili uliofanywa haukuwa mzuri, sasa
wanavuna matokeo ya usajili ambao haukukidhi mahitaji ya klabu kubwa kama
Simba" anasema kiungo mshambulizi wa zamani wa timu hiyo, Ulimboka
Mwakinge ambaye alifunga magoli matatu katika hatua ya robo fainali ya michuano
ya ligi ya mabingwa Afrika mwaka, 2003.
ULI, mchezaji aliyekuwa na kasi,
nguvu, chenga na maarifa binafsi awapo uwanjani anaweza kuonekana ni mnafiki
kwa maneno yake hayo lakini ndiyo ukweli ulivyo. Mchezaji huyo wa zamani wa
timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars ni kama amefikisha ujumbe mzito kwa
klabu hiyo kuachana na kamati zake za usajili na kuwatumia ' ma-scout' kama
sehemu sahihi kuwatafuta wachezaji sahihi ambao wataendana ki-mfumo na
ki-utamaduni wa kiuchezaji wa klabu.
" Tatizo la Simba hivi
lilianzia katika usajili, kwa maana kwamba walisajiliwa wachezaji wasio na
hadhi ya kuichezea timu hiyo". Simba imekuwa na matokeo yasiyoridhisha
msimu huu kwani wameshinda mara nne tu katika michezo 15 waliyocheza. Ikiwa
tayari imepoteza michezo mitatu na kutoa sare mara nane mabingwa hao mara 19 wa
kihistoria wa Bara wamezidiwa alama 11 na timu iliyo kileleni. Yanga SC, vinara
wa ligi hiyo tayari wamepoteza michezo miwili msimu huu, yote katika viwanja
vya ugenini.
Kagera Sugar ambayo iliifunga Yanga
mjini Bukoba ilikuwa timu ya kwanza kuifunga Simba katika uwanja wa Taifa, Dar
bs Salaam msimu huuh kisha Mbeya City ikafuatia. Baada ya kipigo cha tatu
katika msimu na cha kwanza ugenini msimu huu kutoka kwa Stand United wiki
iliyopita, Simba ni kama haina uwezo wa kushinda ubingwa ambao waliupata kwa
mara ya mwisho msimu wa 2011/12 kwa kuwa wamekuwa na matokeo mabaya zaidi
katika uwanja wa nyumbani huku wakiwa hawana uhakika wa kupata ushindi katika
viwanja vya ugenini.
0 comments:
Post a Comment