
TAKWIMU za magoli mpaka sasa katika michuano ya ligi kuu soka Tanzania bara zinaonesha kuwa klabu za Ndanda fc na Stand United zimefungwa magoli mengi zaidi kuliko timu yoyote ile ya VPL.
Ndanda fc wamefungwa magoli 18 katika mechi zao 15 walizoshuka dimbani na wao wametikisa nyavu za wapinzani mara 13.
Stand United ya Shinyanga nayo imefungwa magoli 18 na kufunga magoli 13 katika mechi 15 walizocheza sawa na ndugu zao 'Mtwara' kuchele waliopanda ligi kuu pamoja msimu huu.
Ndanda fc imeshinda mechi 4, imetoa sare 4 na kufungwa mechi 7 na miongoni mwa timu zilizopoteza mechi nyingi zaidi sawa na Mgambo JKT waliofungwa mechi 7 pia.
Stand United wameshinda mechi 3, wametoa sare 6 na kufungwa mechi 6.
Timu za Simba na Prisons zimeshikilia rekodi ya kutoa sare msimu huu ambapo kila timu imetoa sare 8.
Simba wapo nafasi ya nne wakiwa na pointi 20 baada ya kushuka dimbani mara 14.
Mnyama ameshinda mechi 4, amefungwa 2 na kutoa sare 8.
Prisons wameshinda mechi 1, wamefungwa 4 na kutoa sare mechi 5. Wana pointi 11mkiani baada ya kushuka dimbani mara 13.
0 comments:
Post a Comment