Saturday, February 28, 2015

WEKUNDU wa Msimbazi Simba wanaikaribisha Tanzania Prisons katika mechi ya ligi kuu soka Tanzania bara inayopigwa uwanja wa Taifa, Dar es salaam leo majira ya saa 10:00 jioni.
Mechi ya kwanza mjini Sokoine mwaka jana, timu hizi zilitoka sare ya 1-1.
Simba wanaingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu ya kichapo cha 1-0 walichopata kutoka kwa Stand United juma lilipita uwanja wa CCM kambarage, Shinyanga.
Prisons wao walilazimisha suluhu (0-0) na Azam fc katika uwanja wa mgumu kupata matokeo kwa wapinzani, Azam Complex, Chamazi, Dar es salaam.
Simba wapo nafasi ya nne katika msimamo wakijikusanyia pointi 20 baada ya kucheza mechi 15.
Wajelajela wao wanaburuza mkia wakiwa na pointi 12 baada ya kucheza mechi 15.
Mechi nyingine inapigwa mjini Mbeya ambapo wenyeji Mbeya City wanachuana na Ruvu Shootings ya Pwani.
City wanazisaka pointi tatu muhimu kwa nguvu zote kwani mechi iliyopita walifungwa 3-1 na Yanga.
Huko CCM Kambarage, Shinyanga, Stand United wanaikaribisha Kagera Sugar, wakati CCM Mkwakwani Tanga, Mgambo JKT wanachuana na Coastal Union.

RATIBA HII HAPA

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video