Michuano ya Kombe la dunia inalotarajiwa kuchezwa mnamo mwaka 2022 huko Qatar limepangwa kutimua vumbi kati ya miezi ya November na December, kikosi kazi cha Fifa kimetoa tamko .
Wakuu wa mpira wa miguu wamekutana mjini Doha kujadili juu ya masuala kadhaa ya kuchagua juu ya hali ya majira ya kiangazi endapo yataathiri afya ya wanamichezo na mashabiki wao.
Majira ya kiangazi nchini Qatar hakizidi nyuzi joto 40C na mwezi wa November na mwezi December hushuka na kufikia nyuzi joto 25.
Kikosi kazi hicho kinaongozwa na chief Sheikh Salman bin Ebrahim Al-Khalifa na amesema kwamba michuano hiyo ya kombe la dunia ya mwaka 2022 inapaswa kupigwa kwa siku chache tu .
Pamoja na mipango na kauli mbalimbali tayari kuna utabiri unaoonesha kuwa michuano hiyo inaweza kuanz arasmi mnamo tarehe 26 November na kwisha tarehe 23 December.
Hata hivyo, Fifa imesema haina mpango wa kupunguza muda wa michuano hiyo kutoka timu 32 ama michezo 64 .
0 comments:
Post a Comment