Kiungo wa
zamani wa klabu ya Manchester United na timu ya Taifa ya Uingereza Owen
Hargreaves ameionya klabu hiyo na kusema kuwa haipaswi kumsajili beki wa kati
wa klabu ya Borrusia Dortmund Mats Hummels.
Mats Hummels
Hargreaves alisema beki huyo ambaye amekuwa katika anga za Manchester United kwa muda mrefu, si mtu sahihi kutua katika dimba la Old Trafford kwani bado ni mzito sana katika ukabaji pamoja na kupeleka mashambulizi.

“Sidhani
kama Hummels ni mtu sahihi kujiunga na klabu ya Manchester United kwa sasa
kwani ligi kuu nchini Uingereza ni ligi ngumu na yenye washambuliaji mahili
wenye uchu wa kufumania nyavu, na kwa mfumo ambao anacheza Hummels ataigharimu
klabu,” Hargreaves aliliambia gazeti la BT
Sport.
0 comments:
Post a Comment