NSSF_Real Madrid Sports
Academy.
Baada ya uandikishaji
kwaajili ya kufuzu kujiunga na NSSF_Real Madrid Sports Academy. Awamu
inayofuata ni ya majaribio ambayo itafanyika Jumamosi tarehe 28 Februari 2015
kwenye viwanja vya Karume jijini Dar es Salaam kuanzia saa 12:45 asubuhi.
Majina ya vijana watakao hudhulia awamu hii yamechapishwa kwenye magazeti
ya Mwananchi, Majira na Mtanzania leo
tarehe 27 Februari 2015.
Majina ya vijana watakao hudhulia majaribio ya
awamu nyingine yatachapishwa kwenye magazeti ya wiki ijayo.
Kwa wale walio orodheshwa wanaombwa kufika
kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuanza majaribio.
Pia wazazi au walezi
wanaombwa waambatane na watoto wao wakiwa wamewapatia vifaa vya michezo kama
vile viatu,soksi, Shin guard, kaptula na flana ya michezo, maji na gharama za
usafiri wajitegemee.
0 comments:
Post a Comment