Uongozi wa klabu ya Simba pamoja na wanachama, kesho jumapili Machi 1, wanatarajia kukutana katika mkutano wa klabu unaotambuliwa na katiba ya Mabingwa hao wa zamani wa ligi kuu ya Tanzania bara ili kujadili maswala yanayoihusu timu hiyo.
Mkutano huo ambao ulikuwa ufanyike toka mwezi Desemba 2014 ikashindikana kutokana mambo kuingiliana, sasa utafanyika kwenye Ukumbi wa Bwalo la Polisi Oysterbay jijini Dar es salaam ukiwa na lengo la kusawazisha matatizo yaliyopo kwenye klabu hiyo.
Akiongea leo, Rais wa klabu ya Simba Evance Aveva amesema kuwa mkutano huo utakuwa na ajenda moja tu ‘Kujadili mwenendo wa timu katika mbio za ligi kuu’ ambapo unatarajia kuanza majira ya saa nne asubuhi.
Leo jioni Simba SC simba wameshinda mabao 5-0 dhidi ya Prisons katika mechi ya ligi kuu iliyopigwa uwanja wa Taifa, Dar es salaam.
0 comments:
Post a Comment