Samatta alikwenda kufanya majaribo CSK Moscow ya Urusi, lakini hakufanikiwa baada ya kupata majeruhi ya kifundo cha mguu
Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam,
Mshambulizi wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana
Samatta ameweka wazi kuwa ataachana na mabingwa mara nne wa kihistoria wa
Afrika, TP Mazembe mara baada ya kumalizika kwa mkataba wake. Akizungumza na
mwandishi wa mtandao wa www.shaffihdauda.co.tz muda mfupi uliopita mshambulizi huyo wa Taifa Stars amesema
kuwa hana furaha katika timu hiyo ya Congo.
Samatta ambaye alipata nafasi ya kufanya
majaribio katika klabu ya CSKA Moscow ya Urusi mwezi uliopita amepewa ofa
nyingi barani ulaya na kama ataendelea kuchezea TP basi atakuwa ni mchezaji
anayelipwa pesa nyingi zaidi barani Afrika. Hivi karibuni kuna vyombo vya
habari ambavyo viliripoti kuwa mchezaji huyo ana furaha kuendelea kuichezea TP
lakini amesema huo ni uzushi mkubwa.
" Sina furaha hapa ( TP Mazembe)
nitaondoka wakati wa majira ya usajili katikati ya mwaka na sitaongeza
mkataba" anasema Samatta. Ni wapi anakwenda, nini kinachomuondoa TP
Mazembe, tafadhaLi endelea kufuatilia mtandao huu wa www.shaffihdauda.co.tz...
Utapata kujua wapi mchezaji huyo anakwenda. Je, tayari ameruhusiwa na Katumbi
Moies mmliki wa TP?.....
0 comments:
Post a Comment