Monday, February 2, 2015


Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
Kikosi cha Mbeya City FC kiko Dar es Salaam tayari kwa mechi yake ya mwishoni mwa wiki dhidi ya JKT Ruvu Uwanja wa Azam jijini haoa.

Msemaji wa Mbeya City FC, Dismas Ten amesema kikosi chao kimetua mapema jijini hapa kikitokea mjini Morogoro ambako kililala 1-0 dhidi ya kikosi cha kocha Adolf Richard cha Polisi Moro.

"Ligi ya msimu huu ni ngumu, timu zimejiandaa vizuri. Tumekuja mapema hapa Dar es Salaam ili tujiandae kwa mechi yetu inayofuata dhidi ya JKT Ruvu," amesema Ten.

JKT Ruvu Stars inayonolewa na kocha wa zamani wa Yanga SC, Fred Felix Minziro, ambacho kiko nafasi ya tano katika msimamo wa Ligi Kuu ya Bara kikiwa na pointi 18 sawa na Mtibwa Sugar na Polisi Morogoro zilizopo nafasi za tatu na nne, kiliishika kwa suluhu Mbeya City FC katika mechi yao ya kwanza msimu huu iliyopigwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini Mbeya Septemba 14 mwaka jana.

Mbeya City FC inayonolewa na kocha bora wa msimu uliopita, mzawa Juma Mwambusi, iko nafasi ya tisa ikiwa na pointi 15 baada ya mechi 12. 

Timu hiyo ya Jiji la Mbeya ina mechgi moja ya kiporo dhidi ya Yanga SC ambayo itapigwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine Februari 21.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video