MABINGWA wa ligi kuu Tanzania bara, Azam fc
wamemaliza ziara yao nchini Congo DR ambako wameshiriki michuano ya Mazembe
inayoendelea mjini Lubumbashi.
Azam walianza kwa kufungwa goli 1-0 na TP Mazembe,
wakatoka sare ya 2-2 na Zesco United ya Zambia na leo wamefungwa 1-0 na Don
Bosco.
Katibu Mkuu wa Azam fc, Idrissa Nassor ‘Father’
amesema kikosi cha Azam kitatua kesho jijini Dar es salaam tayari kwa
maandalizi ya mechi ya ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Polisi Morogoro
itayopigwa uwanja wa Jamhuri mwishoni mwa wiki hii.
“Tutarudi kesho saa mbili asubuhi, tutarudi
Chamazi na kuendelea na mazoezi kuelekea mechi ya jumamosi Morogoro dhidi ya
Polisi Morogoro. Baada ya hapo tutacheza na Mtibwa Sugar”. Amesema ‘Father’ na
kusisitiza: “Mazoezi ya Congo yalikuwa maalumu kwa mechi za ligi ya mabingwa,
tumejifunza mengi na tunatarajia kufanya vizuri”.
0 comments:
Post a Comment