
Mtu mweusi akijaribu kuingia kwenye treni, lakini alizuiwa na mashabiki waliokuwa wakisafiri kwenda kutazama mechi mjini Paris.
VIDEO ya kushangaza ikiwaonesha mashabiki wa Cheslea mjini Paris wakimzuia abiria mwenye rangi nyeusi 'Mwafrika' kuingia katika treni la Metro.
Mashabiki hao walikuwa wanaelekea uwanja wa Parc des Princes kushuhudia mechi ya hatua ya 16 baina ya PSG na Chelsea.
Treni liliposimama katika kituo cha Richelieu-Drouot walimzuia kwa kumsukuma kwa nguvu asiingie ndani ya treni na moja kwa moja ulionekana kuwa ubaguzi wa rangi.
Taarifa zinasema mamlaka zinazohusika ndani ya Chelsea zinafanya uchunguzi wa tukio hilo na mashabiki wao wakibainika kuwa na tiketi za msimu watafungiwa kuingia uwanjani kama fundisho kwa wengine.

Mtu mweusi akijaribu kubishana na mashabiki waliomzuai kuingia ndani ya treni

Jamaa akaishia kusukumwa vibaya na wabaguzi hao wa rangi
0 comments:
Post a Comment