Friday, February 27, 2015

Julio (kulia) akiwapa darasa wachezaji wa Coastal Union

MAZOEZI ya siku mbili aliyosimamia kocha wa Mwadui fc na sasa kocha msaidizi wa muda wa Coastal Union, Jamhuri Mussa Kiwhelo yameongeza morali kubwa kwa wachezaji kuelekea mechi ya kesho ya ligi kuu soka Tanzania bara dhidi ya wenyeji Mgambo JKT.
Timu hizi mbili zinazotumia uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga zitachuana kuanzia majira ya saa 10:00 jioni.
Afisa habari wa Coastal Union, Oscar Assenga ameuambia mtandao huu muda mfupi uliopita kuwa mazoezi ya Julio ni mazito na yamewapa imani kubwa ya kufanya vizuri mechi zijazo.

"Tayari mazoezi mazuri yameshaanza baada ya Julio kuungana nasi akiwa kocha msaidizi na lengo ni kuhakikisha tunafanya vyema mzunguko huu wa pili wa ligi kuu ya Vodacom" Amesema Assenga na kuongeza: "Tayari Julio amekwishaanza kazi kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Mgambo na tuna uhakika wa kuibuka na ushindi".

Ujio wa Julio ameongeza kitu gani kiufundi na kimbinu ndani ya Coastal Union?

Assenga anaibu: "Kikubwa kilichoongezeka ni namna ya ufundishaji, unajua Julio ni miongoni mwa makocha wanaofanya vizuri katika medani ya soka, kikubwa alichofanya ni kuwajenga wachezaji kisaikolojia na kuwarudisha katika hali ya kawaida kama ilivyokuwa. Katika mazoezi ya siku mbili aliyofanya hapa Tanga katika siku hizi mbili yalikuwa ni mazito. Tunaamini kasi hii tukichanganya na kasi ya kocha mkuu tutafanya vizuri."

Kocha mkuu wa Wagosi wa Kaya, Mkenya, James Nandwa anasemaje kuletewa Julio?

Assenga anasema: "Kocha mkuu James Nandwa amepongeza uongozi kwa  kumchukua Julio na ameahidi kushirikiana naye ili kuweza kupata mafanikio".
Katika msimamo wa ligi kuu, Coastal Union wanashika nafasi 7 wakijikusanyia pointi 19 katika mechi 16 walizocheza.
Mgambo JKT wao wapo nafasi ya pili kutoka mkiani wakijikusanyia pointi 17 katika mechi 14 walizocheza mpaka sasa.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video