Kopunovic (kushoto) akiwa na Msaidizi wake, Matola
KOCHA mkuu wa Simba, Mserbia Goran Kopunovic amerudia tena kusisitiza kuwa msaidizi wake, Seleman Abdallah Matola ni kocha mwenye uwezo mkubwa na anatamani kuona anaendelea kukua kufikia kiwango cha kuwa na falsafa yake ya kufundishia mpira.
Akizungumza na mtandao huu jana katika mazoezi ya Simba yanayofanyika uwanja wa Bweni JKT kujiandaa na mechi ya jumamosi ya ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons, Goran alisisitiza kuwa Matola ni gwiji wa klabu ya Simba, hivyo Simba inahitaji kuthamini watu kama hao.
“Nilikutana naye kwa mara ya kwanza kule Zanzibar,
kutoka siku ya kwanza mpaka leo najisikia vizuri kuwa naye, tuna ushirikiano
mzuri, mawasiliano ni mazuri, pia anafanya kazi nzuri wakati wa mazoezi na ni
mtu mwenye malengo”.
“Kiukweli siku moja nitaondoka Tanzania, maombi
yangu kwa mtu huyu ni kumuona anaendelea kufanya kazi, anaendelea kukua,
anakuwa na falsafa ya kufundisha mpira kwasababu ni gwiji wa klabu, yeye ni Simba,
amecheza mechi nyingi za Simba, anameshinda makombe mengi, labda kuna mashabiki
wa Simba hawampendi, lakini yeye ni Simba, Matola ni Simba”.
“Uzoefu wangu na yeye ni pale tunapotembea maeneo
mengi, watu wengi wanamjua yeye ni nani, Simba inahitaji kuwa na mtu kama huyu
ndani yake, ni gwiji wa klabu”. Amesema Goran.
0 comments:
Post a Comment