WAWAKILISHI wengine wa Tanzania ligi ya mabingwa Afrika, KMKM ya Zanzibar wanashuka dimbani kuchuana na Al Hilal ya Sudan katika mechi ya marudiano inayopigwa leo jioni uwanja wa Amaan Zanzibar.
Mechi ya kwanza iliyopigwa Sudan, KMKM walifungwa 2-0.
Ili kusonga mbele Kikosi Maalumu cha Kuzuia Magendo FC kinahitaji ushindi wa mabao 3-0.
Kama watashindwa kupata matokeo hayo, basi washinde 2-0 ili mshindi apatikane kwa mikwaju ya penalti.
Kesho jumapili katika uwanja wa Amaan, Polisi FC ya hapa visiwani Zanzibar itachuana na CF Mounana ya Gabon katika mechi ya marudiano ya kombe la Shirikisho.
Polisi wana mlima mkubwa wa kupanda kwani mechi ya kwanza walifungwa 5-0 nchini Gabon.
Kama wahaitaji kusonga mbele wanahitaji ushindi wa mabao 6-0 au watoke sare ya 5-5 na kusubiri hatima yao katika mikwaju ya penalti.
0 comments:
Post a Comment