Friday, February 27, 2015

Deus Kaseke (kushoto) akiwa Richard Peter.
 KIUNGO  mshambuliaji nyota wa Mbeya  City  Fc, Deus Kaseke  amesema kikosi cha City bado kina nafasi ya kufanya vizuri na kushika nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara inayondelea  kutimua vumbi hivi sasa kwenye viwanja mbalimbali.
Akizungumza  na mbeyacityfc.com, Kaseke amesema kuwa hali ilivyo kwenye msimamo wa ligi hivi sasa timu zote bado ziko kwenye nafasi ya kufanya vizuri kwa sababu hazijapishana pointi nyingi pia uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa bado siyo mkubwa.
“Nahisi bado tuna nafasi ya kufanya vizuri na kupata nafasi za juu, ukiutizama msimamo wa ligi hivi sasa timu nyingi hazijapishana sana, kama utafanikiwa kupata matokeo kwenye michezo miwili unakuwa tayari ushasogea kwenye nafasi za juu, naamini City itafanikiwa kutoka hapo na kurudi kwenye nafasi  hizo, kama wachezaji ndani ya kikosi  bado tuna ari kubwa ya kufanya hivyo” alisema.
Katika hatua nyingine Kaseke alisema mchezo wa jumamosi dhidi ya Ruvu Shooting utatoa taswile ya kile ambacho City itakipata kwenye michezo miwili ijayo katika msimamo wa ligi kabla ya kuivaa Azam Fc kwenye mchezo mwingine wa ligi hiyo utakaochezwa Chamanzi Complex jijini Dar.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video