Mlinda mlango wa City, Hanington Kyalesebula amesema yuko tayari kuitumikia timu yake kwa moyo mmoja ili kurejesha kile kilichokuwa kimekosekana kwenye milingoti mitatu ya goli la City.
Akizungungumza na mbeyacityfc.com mapema leo mara baada ya kumalizika kwa mazoezi ya asubuhi kwenye uwanja wa Sokoine Hanington amesema kuwa anafahamu hamu na imani waliyonayo mashabiki wa Mccfc juu yake hasa baada ya matokeo mabaya kwenye mchezo uliopita wa ligi kuu ya bara dhidi ya Yanga na kuahidi kuwa atafanya kazi vizuri.
“Nashukuru niko hapa sasa, ndani ya soka kuna mambo mengi lakini kilicho kichwani kwangu hivi sasa ni kufanya kazi yangu kwa nguvu na moyo wote, najua mashabiki wa City wana kiu ya kuona nitawawakilisha vipi uwanjani hasa baada ya matokeo mabaya kwenye mchezo uliopita,sina mengi ila ninachoweza kusema kwao ni kuwa nipo tayari na wasihofu nitafanya kazi” alisema Hanington.
Haningtony Kyalesebula Kushoto.
Golikipa huyo raia wa Uganda amejiunga na City msimu huu ikiwa ni baada ya kucheza kwa mafanikio kwenye kikosi cha Kagera Sugar msimu mmoja uliopita kabla ya kurudi kwao Uganda.
0 comments:
Post a Comment