MLINZI wa kushoto wa Mbeya City Fc, Hamad Kibopile amesema kupoteza mchezo uliopita wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara dhidi ya Yanga ni jambo ambalo tayari limeshapita kilichopo sasa ni kutizama mchezo ujao dhidi ya Ruvu Shooting unaotarajiwa kuchezwa kwenye uwanja wa Sokoine mwishoni mwa juma hili.
Akizungumza na mbeyacityfc.com mapema leo Kibopile aliyejizolea umaarufu mkubwa kutokana na ‘style’ yake ya kurusha mpira amesema hakuna aliyetarajia kama City ingepoteza mchezo huo miongoni mwa wachezaji na mashabiki lakini kwa kuwa mchezo wa soka una mambo mengi matokeo yakaja tofauti.
“Kwa namna ambavyo timu ilikuwa imeandaliwa hakukuwa na yoyote kati yetu alifikiri tungepoteza mchezo huo hali ilikuwa hivyo pia kwa pia kwa mashabiki wetu, lakini soka lina mambo baada ya dakika 90 matokeo yalikuwa mabaya kwetu, kwangu mimi hayo yameshapita kilichopo sasa ni kuutizama mchezo ujao, hatuhitaji kitu kingine zaidi ya matokeo imani yangu kubwa kuwa hakuna aliyekata tamaa tutapambana mpaka dakika ya mwisho kwa ajili yetu na pia mashabiki wetu” alisema Kibopile.
Akiendelea zaidi Kibopile aliwashukuru mashabiki wa City popote walipo kwa kuisaapoti timu yao na kuwataka kuendelea na moyo huo kwa sababu City bado itabaki kuwa City licha ya kupoteza mchezo dhidi ya Yanga.
0 comments:
Post a Comment