Samatta (kushoto) alikwenda kufanya majaribo CSK Moscow
Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam,
Mshambulizi wa kimataifa wa
Tanzania, Mbwana Samatta ameweka wazi kuwa ataachana na mabingwa mara nne wa kihistoria
wa Afrika, TP Mazembe mara baada ya kumalizika kwa mkataba wake.
Akizungumza na
mwandishi wa mtandao wa www.shaffihdauda.co.tz muda mfupi uliopita mshambulizi huyo wa Taifa Stars amesema
kuwa hana furaha katika timu hiyo ya Congo.
Samatta ambaye alipata nafasi ya kufanya
majaribio katika klabu ya CSKA Moscow ya Urusi mwezi uliopita amepewa ofa
nyingi barani ulaya na kama ataendelea kuchezea TP basi atakuwa ni mchezaji
anayelipwa pesa nyingi zaidi barani Afrika.
Hivi karibuni kuna vyombo vya
habari ambavyo viliripoti kuwa mchezaji huyo ana furaha kuendelea kuichezea TP
lakini amesema huo ni uzushi mkubwa.
" Sina furaha hapa ( TP mazembe)
nitaondoka wakati wa majira ya usajili katikati ya mwaka na sitaongeza
mkataba" anasema Samatta, ni wapi anakwenda, nini kinachomuondoa TP
Mazembe,

Haya hapa mahojiano kati ya Mbwana Samatta na mwandishi wa
mtandano huu, Baraka Mbolembole….
www.shaffidauda.co.tz; Samatta kumekuwa na taarifa kwamba licha ya baadhi ya vikwazo unavyokutana navyo
unapopata fursa ya kucheza Ulaya katika klabu yako ya TP Mazembe bado
unafurahia kuwepo ndani ya timu hiyo. Je, ni kweli una furaha kuendelea
kuichezea TP?
Mbwana Samatta; Hahaha, ni uongo huo, sina furaha kuendelea
kucheza hapa na wala sitaongeza mkataba mpya, nadhani nitaondoka wakati wa
usajili ujao wa kiangazi.
www.shaffihdauda.co.tz; Kwa niaba ya wasomaji wa webisite hii ( www.shaffihdauda.co.tz) ningependa
kufahamu nini kilitokea katika majaribio yako CSKA Moscow ya Urusi klabu ambayo
ilikupatia nafasi ya kwenda kufanya majaribio. Ni kweli sababu za majeraha
ndiyo zimekunyima nafasi?
Mbwana Samatta; Kwa kweli suala la majeraha lilikuwa ni
sababu ndogo sana na mahitaji ya CSKA, lakini tatizo lilikuja katika suala la
makubaliano kati ya CSKA na TP. Kiukweli Mazembe walihitaji kiasi kikubwa sana
ambacho ambacho ni vigumu kwa klabu ya ulaya kutoa kwa mchezaji anayecheza
Afrika.
Ukichanganya na sababu za kimkataba ambao umebaki mwaka
mmoja kati yangu na TP ilibidi CSKA washindwe kwa sababu hizo na si majeraha
kwa kuwa walinihati hivyohivyo. Baada ya hapo nilizungumza na klabu kuhusu ‘
future’ yangu, so nasubiri muda ukifika nitaingia nao makubaliano flani hata
kabla muda wangu haujakwisha na TP.
www.shaffihdauda.co.tz;
Unamaanisha kuwa bado kuna nafasi kubwa yaw ewe kujiunga na CSKA Moscow?
Mbwana Samatta;
Nafasi ipo ya mimi kujiunga na CSKA pia bosi wa klabu hiyo amekuwa na
urafiki na klabu nyingi za ulaya hivyo kuna uwezekano mkubwa akaninunua kwa
sababu ya klabu nyingine, nadhani umenielewa.

www.shaffihdauda.co.tz;
Kwa nini unaondoka TP Mazembe?
Mbwana Samatta;
Nadhani imetosha kwa sisi kuendelea kucheza barani Afrika, sasa nataka
kuishi katika ndoto zangu.
www.shaffihdauda.co.tz;
Kila mwanasoka huwa na ndoto kubwa, ndoto yako imeegemea wapi kimpira?
Mbwana Samatta;
Napenda kucheza LIGA BBVA, ndoto yangu ni kucheza ligi kuu ya Hispania,
La Liga.
www.shaffihdauda.co.tz;
Miaka minne ndani ya klabu kubwa Afrika TP Mazembe imekufunza nini ukizingatia
ulitoka Tanzania ukiwa U18?
Mbwana Samatta; Kwa kweli nimepevuka kwa kiasi kikubwa
kimpira na kiakili, tayari nimecheza dhidi ya klabu zote kubwa barani Afrika.
Nimepata uzoefu mkubwa sana na kujiamini
kwa kiasi kikubwa. Nashukuru kwa kila kitu ambacho TP wamekuwa
wakiendelea kufanya dhidi yangu. Nimejiiimarisha kutoka mchezaji kijana hadi
kuwa mtu jasiri ndani ya uwanja.
www.shaffihdauda; Je,
umezungumza na mmiliki wa TP, Moise Katumbi kuhusu kuondoka kwako kabla ya
kumalizika kwa mkataba, amesemaje?
Mbwana Samatta; Nilizungumza naye sana tu na amekubaliana
name hivyo muda utakapofika amesema hatokuwa na kipingamizi tena, ataruhusu
niondoke.
Ni mchezaji gani ungependa kupata Interview yake?
0714 08 43 08
0 comments:
Post a Comment