
Dr. Tibohora (kushoto) akiwa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga,Jerry Muro
KATIBU mkuu wa Mabingwa wa zamani wa ligi kuu ya
Soka Tanzania bara, Dar es salaam Young Africans, Dr. Jonas Tibohora, amesema
kuwa wachezaji wengi hasa wa kigeni (Professional Players) wameshindwa kutambua
thamani yao wakiwa Uwanjani kitu ambacho kinasababisha kushindwa kuwatofautisha
na wazawa.
Akizungumza na Mtandao huu juu ya matokeo ya kutoridhisha kwa timu kubwa za VPL licha ya
kuwa na uwekezaji wa hali ya juu kwenye ligi, Katibu huyo ambaye alichukua
mikoba ya Beno Njovu, amesema kuwa inatakiwa iwepo tofauti kubwa kati ya
mchezaji wa Kimataifa na mchezaji wa ndani, lakini kutokana na viwango visivyoridhisha
kwa wachezaji wa kigeni imekuwa ngumu kutofautisha kati ya timu kubwa na ndogo
zinapokutana kwenye mechi za ligi.
Dr. Tibohora amekili kuwa klabu kubwa za Tanzania bara,
Simba, Yanga na Azam, zimewekeza sana kwa kununua wachezaji na makocha wa
kigeni lakini bado hazioneshi tofauti na timu nyingine zinazotumia makocha na
wachezaji wa ndani pekee wanapokuwa Uwanjani.
“Taaluma na maadili ya wachezaji wetu bado inakuwa
sio nzuri, Ukiangalia wachezaji wa timu kubwa wanapocheza na timu ndogo
unashindwa kutofautisha timu kubwa ni ipi na ndogo ni ipi” Amesema Dr. Tibohora.
Timu za Azam FC, Yanga SC, Simba SC ndio timu
ambazo zinaongoza kwa kuwa na makocha wa kigeni na wachezaji kutoka nchi za nje
lakini matokeo ya Uwanjani hasa zinapokutana na timu kama Ndanda, Stand United
na Polisi Morogoro bado unashindwa kutofautisha Kiwango cha wachezaji wa vigogo
hao pamoja na hizi timu Changa.
.jpg)
Mshambuliaji wa Yanga, Mrundi Amissi Tambwe (kulia) akishangilia moja ya goli aliloifungia klabu yake
Licha ya kudai kuwa hata uongozi wa klabu za Tanzania bara zinakosea katika
njia za kutafuta na kusajili wachezaji wa kigeni lakini Katibu huyo ametupa
zigo la lawama kwa wachezaji wa Kigeni akisema kuwa ni lazima waonyeshe tofauti
na thamani yao kama Maprofesional kweli.
“Tatizo ni la wachezaji wetu, Bado hawajaelewa
nini maana ya Professionalism, Unapokuwa umepewa kazi lazima ujue namna gani uwe kama mchezaji wa kulipwa, Ni
lazima kuwe na tofauti kati ya mchezaji anayelipwa Milioni tano na yule
anayelipwa Laki tatu” Ameongezea Dr. Tibohora.
Kwa upande wake Meneja wa Klabu ya Azam FC,
Jemedali Said, amesema kuwa kubweteka kwa wachezaji wa timu kubwa na kukamia
kwa timu ndogo ndio kimekuwa sababu ya kufanya utofauti kati ya Simba, Yanga ,
Ndanda, Ruvu Shooting na Mgambo JKT usionekane pindi wanapokutana katika
mchezo.
Jemedali amesema kuwa, Timu ndogo za VPL zimekuwa na kanuni ya kuzikamia timu
kubwa kitu kinachosababisha wachezaji wa timu kubwa washindwe kucheza katika
viwango vyao.
Kipre Tchetche ni miongoni wa wachezaji wa kigeni wa Azam fc
Meneja huyo ambaye amewahi kuichezea Yanga amedai
kuwa, wachezaji wa timu kubwa wamekuwa na dharau pindi wanapokutana na timu changa wakijua muda wowote watapata bao kinyume na wapinzani wao ambao wanakuja
kupambana mwanzo mwisho.
“Upinzani uliopo kwa timu hizi tatu kubwa, wachezaji
wanaingia Uwanjani wakijua wao ni Nyota, wana viwango vikubwa kitu
kinachopelekea washindwe kucheza katika kiwango cha juu, Kwa matokeo yake sasa
ukikuta timu ndogo inajituma kwa kiwango kinachotakiwa ndio utaona wanafungwa
au kutoa sare” Amesema Jemedali Said Meneja wa Azam FC, huku akiongezea kuwa
hata Azam FC kufungwa na Ndanda FC katika ligi ilikuwa ni katika misingi hiyo
ya wachezaji kudharau.
0 comments:
Post a Comment