JUVENTUS imetumia vyema uwanja wake wa nyumbani wa Juventus Stadium kuwaadhibu 2-1 Borrusia Dortmund katika mechi ya kwanza ya UEFA Champions league.
Carlos Tevez aliifungia Juve goli la kuongoza katika dakika ya 13', lakini Marco Reus alisawazisha dakika tano baadaye.
Dakika mbili kabla ya mapumziko, Alvaro Morata aliandika bao la pili lililoduma mpaka dakika 90' ya mchezo.
Kwa matokeo hayo, Juventus wanahitaji suluhu ugenini au ushindi ili kusonga mbele.
Kama watafungwa 1-0 watatoka kwasababu Borussia wamefunga goli la ugenini.
0 comments:
Post a Comment