Kocha Msaidizi wa Coastal Union,Jamhuri Kihwelo "Julio"kulia akisisitiza jambo mazoezini jana mara baada ya
kuwasili mkoani Tanga kuifundisha timu hiyo. Kushoto ni Kocha Mkuu James Nandwa ,Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Coastal Union,Albert Peter,Katibu Mkuu Coastal Union,Kassim El Siagi na Meneja wa Coastal Union Akida Machai.
Kocha Msaidizi wa Coastal Union ,Jamhuri Kihwelo "Julio"akizungumza na viongozi wa Coastal Union mara baada ya kuwasili mazoezini jana. Picha kwa Hisani ya Coastal Union
KOCHA wa klabu ya Mwadui fc, Jamhuri kihwelo "Julio" ametua katika klabu ya Coastal Union ya jijini Tanga kwa mkopo mpaka mwisho wa msimu huu ambapo atakuwa klabuni hapo kama kocha msaidizi.
Imeripotiwa kuwa kocha huyo amechukua uamuzi huo kutokana na urafiki wake wa karibu na klabu hiyo,pia analengo la kuinua kiwango cha timu hiyo kinachoonekana kuyumba msimu huu.
Coastal Union ambayo iko chini ya kocha mkenya James Nandwa imekuwa ikisuasua kunako ligi kuu Tanzania bara na kwa sasa inashika nafasi 7 ikiwa na pointi 19 katika ligi hiyo.
Julio amekuwa kocha tishio nchini na sasa ameipandisha daraja timu ya Mwadui na kutwaa ubingwa wa ligi daraja la kwanza baada ya kuitandika African sports katika mchezo wa fainali uliopigwa jumapili iliyopita kwenye uwanja wa Azam Complex huko Chamanzi jijini Dar es salaam.
0 comments:
Post a Comment