Monday, February 2, 2015



Beki wa pembeni wa klabu ya Fc Barcelona Jordi Alba ameibuka na kumtetea Mshambuliaji wa klabu hiyo aliyesajiliwa kutoka katika klabu ya Liverpool Luis Suarez, licha ya nyota huyo kushindwa kung'ara katika mitanange ya Ligi Kuu Nchini Uhispania La Liga pamoja na kombe la Mfalme Copa Del Rey.


Alba amesema licha ya Suarez kutoonyesha cheche zake za kufumania nyavu tangu ajiunge na klabu hiyo, bado anaitaji muda zaidi kwa ajili ya kuzoea mfumo wa uchezaji wa klabu hiyo pamoja na kuongeza juhudi zaidi ili aweze kurudi katika hali yake ya zamani.


"Nafikiri licha ya Suarez kutofumania nyavu mara kwa mara katika mechi za ligi kuu pamoja na klabu bingwa barani Ulaya bado ni usajili bora uliofanywa na klabu ya Fc Barcelona, Suarez anaitaji muda zaidi kuzoea Mfumo wa timu pamoja na kuongeza juhudi zaidi katika mazoezi," alisema Alba.



0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video