Beki wa klabu ya Manchester United John Evans amesema licha
ya klabu hiyo kutofanya vizuri katika mechi zake za hivi karibuni kwa kukubali
kupoteza na kusuluhu mechi kadhaa katika ligi kuu nchini uingereza, lakini safu
ya ushambuliaji ya klabu hiyo ipo katika hali nzuri inayoridhisha na
kuburudisha.
Evans alisema wachezaji wa klabu hiyo tayari wameanza kuzoea
mfumo wa kocha mholanzi Luis Van Gaal wa
3-5-2,United ililazimika kurudiana mchezo na klabu ya Cambridge United
katika kombe la FA baada ya kutoka suluhu katika mchezo wa kwanza
ugenini na nyumbani kufanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli matatu kwa bila
katika dimba la old Trafford.
“Nafikiri tupo vizuri sana hususani katika safu ya ushambuliaji
ikiongozwa na naodha Wayne Rooney,Robin Van Persie,Angel Di Maria na Radamel
Falcao kwa kweli inatumbuiza sana klabu yetu licha ya kusuluhu michezo mingi,”
alisema Evans
0 comments:
Post a Comment