Tuesday, February 3, 2015

Jerome Champagne ameondolewa katika mbio za uraisi wa shirikisho la soka ulimwenguni FIFA kufuatia kukosa kutimiza idadi ya watu wa kumuunga mkono


Hata hivyo, Mfaransa huyo (Champagne) amebainisha kuwa kuondolewa huko kumetokana na baadhi ya mashirikisho ya nchi mbalimbali kuogopa ‘kulipizwa’ endapo watamuunga mkono.

Mnamo mwezi Januari ya mwaka ulopita Champagne alitangaza azima yake ya kujitosa katika chaguzi hiyo ya FIFA ambayo kwa sasa raisi wake ni Sepp Blatter, lakini amejikuta akiambulia kukubaliwa na nchi tatu tu ilihali zinahitajika tano ili kuingia katika mchuano wa kupigiwa kura. Champagne amesema ni wazi shirikisho la soka barani ulaya (UEFA likishirikiana na vyama mbalimbali walikusudia kumuondoa.

"Nasikitika sana kutangaza kukosa barua tano za udhamini ili kuweza kuidhinishwa kama mmoja wa wagombeea wa uchaguzi hapo baadaye, mwezi mei 29 mwaka huu" alisema. "ninayashukuru sana mashirikisho matatu yaliyoniunga mkono pia nawashukuru maraisi wote walioeleza kwa uwazi na urafiki kwamba wasingeweza kufanya hivyo pamoja na kufurahishwa na mipangilio yangu" Aliongeza

"Ni wazi kumekuwa na ushirikiano wa kuniangusha sababu nilikua mgombea pekee wa kujitengeme. Matukio ya usiri ya kuwaunga mkono miongoni mwa wagombea yamenifanya nikose udhamini hususani barani ulaya! "ajenda ilofichika au isofichika iko wazo, huu ni wakati ambao FIFA inahitaji umadhubuti wa hali ya juu kuliko kipindi chochote kutimiza malengo toka 1998!

"Pia ni wazi lengo lilikuwa kuwawezesha watu wa Ulaya magharibi ili watimize azima yaoo kwa kile wanachokikosa." Jerome Champagne pia amebainisha sababu lukuki kwanini hawezi tena kuwania uraisi wa FIFA.

"Pia ningeweza kuwa mgombea kwa kuzingatia kanuni za kale lakini si baada ya mabadiliko mapya ya mwaka 2013 yaliyotokana na shirikisho la ulaya (UEFA). Ila pamoja kushindwa kutimiza lengo, bado sijisikii uncungu sana kwani tayari naelewa namna soka linavyoendeshwa”


Mapema jana (jumatatu) shirikisho la soka ulimwenguni FIFA lilithibitisha kuwa watakaowania kiti hicho ni pamoja na raisi wa sasa Sepp Blatter, anayewania awamu ya tano ya uongozi huo hapo mwezi mei, atayekabiliana na Prince Ali Bin Al-Hussein wa Jordan, mkurugenzi mkuu wa shirikisho la soka la uholanzi Michael van Praag sambamba naye nyota wa kimataifa toka ureno Luis Figo. Hata hivyo kabla ya uchaguzi huo ndani ya siku kumi zijazo utafanyika uchunguzi wa uadilifu miongoni mwa wagombea.

Mgombea mwingine David Ginola pia alishajiondoa mapema baada ya kukosa kuungwa mkono na mashirikisho matano ya Soka.

Champagne amekuwa akifanya kazi mpaka 2010, alipolazimika kuachia ngazi kama mkurugenzi kwa kile kilichoonekana tayari alikuwa na lengo la kuwania uraisi huku akishindwa kutimiza wajibu wake ipasavyo. 

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video