Klabu
ya Real Madrid chini ya Kocha Carlo Ancelloti imedhibitisha kuwa kiungo
mshambuliaji wa klabu hiyo na timu ya taifa ya Colombia James Rodriguez
amevunjika mfupa katika mguu wake wakipambana na klabu ya Sevilla
katika mchezo wa ligi, ambapo Real Madrid ilifanikiwa kuibuka na ushindi
wa magoli mawili kwa moja.
Mabingwa hao watetezi wa kombe la klabu bingwa Barani Ulaya
pia wapo njia panda kuhusu beki wao wa kati Sergio Ramos, ambae nae
alipata jeraha la nyama za paja katika mchezo huo na huenda akaukosa
mchezo wao dhidi ya majirani Atletico Madrid wikiendi hii.
James
ambae alifungua kalamu ya magoli katika huo, alikimbizwa hospitali kwa
uchunguzi zaidi baada ya kuumia na sasa atakuwa nje kwa takribani miezi
miwili.
0 comments:
Post a Comment