
Mshambulizi wa Paris Saint-Germain, Zlatan Ibrahimovic anaamini wataitupa nje Chelsea
MSHAMBULIAJI wa Paris Saint-Germain, Zlatan Ibrahimovic anaamini timu yake ina nafasi nzuri zaidi ya kutinga robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Wapinzai wao Chelsea walipata faida ya goli la ugenini katika sare ya 1-1 jana usiku uwanja wa Parc des Princes, shukuruni kwa bao la Branislav Ivanovic, lakini Ibrahimovic anajiamini kuwa kikosi chake kitapata matokeo mazuri Stamford Bridge.
Akizungumzia sare ya jana dhidi ya vinara wa EPL, Chelesea, Ibrahimovic amesema: "Tuko katika nafasi nzuri ya kusonga mbele. Mchezo bado uko wazi".

Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho akisalimiana na Ibrahimovic baada ya kipyenga cha mwisho
"Tulionesha kuwa tunaweza kutengeneza nafasi nyingi. Sio kazi rahisi ligi ya mabingwa. Wana wachezaji wakubwa. Huu ndio mpira. Tunahitaji kuomba bahati. Ngoja tusubiri kuona kocha atataka tuchezaje mechi ya marudiano". Amesema Ibrahimovic.
0 comments:
Post a Comment