Na Frank .M. Mgunga
LIGI kuu soka Tanzania bara imeendelea kurindima katika viwanja mbalimbali nchini, huku katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam kukipigwa mtanange wa kukata na shoka kati ya klabu ya na wajelajela Tanzania Prisons kutoka Jijini Mbeya.
Iliwachukua Simba takribani dakika 21 kuweza kuandika bao la kwanza kupitia kwa Ibrahim Hajibu baada ya kazi nzuri iliyofanywa na mchezaji raia wa Uganda Emmanuel Okwi.
Simba iliendeleza mashambulizi katika lango la Prisons na kumfanya Hajibu kwa mara nyingine kupachika bao la pili katika dakika ya 34 ya mchezo.
Simba iliendeleza mashambulizi katika lango la Prisons na kumfanya Hajibu kwa mara nyingine kupachika bao la pili katika dakika ya 34 ya mchezo.
Nyota ya mchezaji huyo chipukizi iliendelea kung'ara katika mchezo huo kwa kuandika bao la tatu na kukamilisha"Hat trick" kwa mkwaju wa Penati katika dakika ya 41 ya mchezo baada ya mchezaji wa Tanzania Prisons kuunawa mpira eneo la hatari.
Bao hilo liliwafanya Simba iende mapunziko wakiwa kifua mbele kwa mabao matatu kwa bila.
Bao hilo liliwafanya Simba iende mapunziko wakiwa kifua mbele kwa mabao matatu kwa bila.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kushambuliana kwa kasi,lakini Simba walionesha kuwa wamepania kuibuka na ushindi katika mchezo huo kwa kuliandama lango la Tanzania Prisons kwa kasi zaidi na kumsababisha mchezaji wa Prisons Nurdin Chona kukubali lawama alipooneshwa kadi ya pili ya njano na kutolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu mbaya Ramadhan Singano "Messi".
Emmanuel Arnold okwi aliwaamsha mashabiki wa Simba katika dakika ya 74 ya mchezo baada ya kuachia shuti kali lililomshinda mlinda mlango wa Prisons na kuiandikia Simba bao la nne, na dakika sita baadaye Ramadhani Singano akahitimisha karamu ya magoli kwa Wekundu wa msimbazi baada ya kufunga bao la tano akipokea pasi safi kabisa kutoka kwake Emmanuel Okwi.
MATOKEO MENGINE
Mbeya City 1 Ruvu Shooting 1
Mgambo JKT 0 Coastal Union 1
Stand United 1 Kagera Sugar 0 (Mechi ameahirishwa dakika ya 80' kutokana na mvua kali aliyoanza kunyesha uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga)
0 comments:
Post a Comment